Askofu Zachari Kakobe ni mwanauamusho wa kimataifa, na mwanzilishi wa Bishop Zachary Kakobe International Ministries (BZKIM), shirika lisilo la kibiashara la kiimani , lililosajiliwa Marekani. Pia ni mwanzilishi na Msimazi Mkuu waFull Gospel Bible Fellowship Church, lenye usajiri wake nchiniTanzania. Anachunga kanisa lenye maelfu ya waumini jijini Dar-Es-Salaam, Tanzania; ambalo ni kanisa mama; ambalo kwalo, anasimamia zaidi ya matawi 400 (matawi), ambayo aliyaanzisha kwa kuyatawanya katika mikoa na wilaya zote za Tanzania bara.
Askofu Zakaria Kakobe ni Mtanzania; alizaliwa siku ya Jumatatu, Juni 6, 1955; huko Kibondo, Tanzania. Safari yake ya kiroho ilianza Jumapili ya Pasaka, Aprili 6, 1980; siku alipozaliwa kiroho wakati mkutano wa Miujiza ya Uponyaji kanisani, vilivyoendeshwa nchini Tanzania na Mwinjiristi mashuhuri wa Kitaifa Askofu Moses Kulola, katika kanisa laTanzania Assemblies of God, Ilala, Dar-Es-Salaam, lililokuwa likichungwa na Mchungaji Titus Mukama. Jioni ile, ujumbe wa kiinjili ulioukuwa ukihubiriwa na Askofu Moses Kulola, ulimfanya Zakaria Kakobe kwenda madhabahuni kuombewa , kwa ajili ya Kuokoka. Alikwenda mbele ya kanisa akilia kwa uchungu waziwazi, na kutubu dhambi zake; akiwa na kusudio halisi toka ndani ya moyo wake , kuacha dhambi, na anasa; na kumpokeaYesu ndani ya moyo wake kuwa Mtawala Mkuu na Mwokozi wake.
Tangu siku hiyo, maisha yake yalibadilika kabisa.Mkewe na marafiki zake waliomfahamu kabla, walishuhudia na kuthibitisha kwamba maisha yake yalikuwa yamebadilika. Alikuwa amezaliwa tena.Alikuwa ni mtu mpya, katika Kristo. Mda mfupi baadae alijiunga na kanisa la Tanzania Assemblies of God, Temeke, Dar-Es-Salaam; kanisa alilokuwa akisali Kwa miaka kadhaa, alikuwa ni mshirika mwaminifu wa kanisa hilo, na mchungaji wake alikuwa ni hayati Callist Masalu, ambaye alikuwa ni Mtumishi wa Mungu mashuhuri nchini Tanzania kwa zaidi ya miongo minne.
Wito wa uchungaji wa Askofu Zakaria Kakobe ulikuwa ni wa kipekee, au kwa lugha rahisi, ulitokea kimiujiza. Mnamo mwaka 1982, Yesu Kristo mwenyewe alimtokea kwa nyakati mbili tofauti sebuleni, kumpa ujumbe Wake wa kumuita kwenye uchungaji. Kwa nyakati zote Yesu alimtokea sebuleni mapema usiku, mapema kabla ya mda wa kulala wakati shughuli za kawaida zilikuwa zikiendelea sebuleni. Katika tukio la kwanza, Yesu alibisha hodi kwenye mlango uliofungwa vizuri, na kabla mda wa kufungua mlango, alipita kwenye mlango ule bila kuufungua.Alivyoingia , taa za sebule zilizima, bila kuzimwa na mtu yeyote, na utukufu Wake ukaangaza. Kisha akakaa na kusema “Msigope, Mimi ni Yesu”. Kisha akasema ya kwamba anamtuma Kakobe kuhubiri Neno Lake.
Aliendelea kusema kwamba, Kakobe, atakuwa Mchungaji wa kundi kubwa la kondoo, na atawatunza na kuwalisha maelfu ya kondoo na wanakondoo; na kwamba atayaangalia makundi mengine mengi ya kondoo. Wakati huohuo, atahubiri Injili kwa mataifa, katika mataifa mengi duniani, huku ishara za uweza na maajabu zikimfuata kokote alikoenda kuhubiri Neno Lake. Aliongea sana kuhusu vitu vingine vihusuvyo mpango wa Mungu kuhusu maisha na uchungaji wa Kakobe, na Akahitimisha kwa kumsihi tena na tena, kuwa mwaminifu kwake hadi mwisho; ili avione vitu vyote hivi vikitimia, ndani ya uchungaji wake. Baada ya hitimisho, hakumpa nafasi ya kujadiliana. Kisha akaondoka kupitia mlango ule ule, kwa namna ile ile, na papo hapo, taa za sebule zikawaka tena zenyewe.
Katika hali ya kushangaza baada ya kupokea ujumbe, Kakobe aliitikia kwa kuukataa wito wa Yesu Kristo. Katika majadiliano ya hisia na mkewe Hellen, Kakobe alimwambia mkewe, “Samahani, siwezi kuwa mhubiri wa msalaba wala mchungaji. Sina mpango kabisa na aina hii ya utumishi. Mpango pekee ni kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa, na kutumia pesa zangu kuendeleza injili ya Yesu Kristo. Si zaidi wala pungufu ya hapo!”.Kwa wakati huo, Kakobe alikuwa akihusika katika misaada ndani ya Kanisa, Tanzania Assemblies of God. Alimsaidia mwinjilisti wa Tanzania, Askofu Moses Kulola, kuanzisha utumishi wa kurekodi na alikuwa akitumia vifaa vyake vya kielektroniki kurekodi jumbe zake za injili na kusambaza tepu za mahubiri kwa wasikilizaji wengi; kwa gharama zake mwenyewe. Alikuwa na jukumu la kusambaza Neno kupitia tepu za mahubiri za Askofu Kulola.
Alikuwa pia ni mwenzi ndani ya utumishi wa Askofu Kulola. Alitakiwa kujitoa kwa kadri ya uwezo wake, kwa ajili ya injili ya Ufalme. Hakuwa kabisa na fikra za kuwa mhubiri wa neno la msalaba katika kanisa lake la Assemblies of God alikokaa, hakuwahi kupangiwa kuhubiri wala kufundisha. Alikuwa ni muumini wa kawaida tu wa kanisa. Alimwambia mke wake,“ Kama Yesu akinipa nafasi ya kujibu wito wake, jibu langu litakuwa, sina nia ya kuja kuwa mchungaji wala mhubiri wa mikutanoni, na nitamwomba anipe uwezo wa kupata mali; ili niwafadhili vya kutosha Wahubiri wa Injili.
Miezi kadhaa baadae, mwaka uleule; Yesu alikuja tena katika makazi ya Kakobe, katika namna ile ile. Katika ujio Wake wa pili, alichukua mda mfupi kuelezea mpango wa Mungu kuhusu maisha ya Kakobe na huduma yake; lakini mara hii kwa msisitizo zaidi; na kisha akahitimisha kwa kusema kwamba itachukua mda mrefu zaidi kwa Yeye kurudi tena katika namna ile; na baada ya hapo akaondoka.
Ujio huu wa pili wa Yesu ulileta maendeleo chanya kwa Kakobe kimwitikio wa wito? La hasha! Kakobe aliendelea na msimamo uleule kwa miaka kadhaa, bila kupunguza. Hadi ikafika mwaka 1987, mnamo mwezi wa kumi na moja, wakati Mwinjilisti wa Kimataifa, mwenye upendo na Afrika, Reinhard Bonnke, aliitisha mkutano wa injili Dar-Es-Salaam, Tanzania. Mkutano huo ulivuta maelfu ya watu kutoka sehemu zote za nchi. Kakobe alikuwa mmoja wa walioongoza mkutano huo. Siku ya mwisho ya mkutano, kulikuwa na uamusho mkubwa wa roho wa Mungu. Watu maelfu walimpokea Yesu , na miujiza mingi ikatokea. Mhubiri alipokuwa akihitimisha, Kakobe alitumia mda kutafakari makundi ya watu, upokewaji mwingi wa Yesu Kristo, na miujiza iliyotokea, ambayo ilimtukuza Yesu Kristo jijini na nchi nzima kwa ujumla. Wakati akitafakari mambo haya, kutokewa mara mbili na Yesu Kristo kulikomtokea sebuleni kwake, miaka mitano nyuma, kukamrudia tena akilini mwake, na ghafla akasikia sauti ndogo tulivu ikisema moyoni mwake na kusema, “Mwanangu, mhubiri sasa yu auaga mkutano, ambao utaendelea kulitukuza Jina Langu, baada ya kuondoka kwake?”Baada ya sauti hii nini kilitokea?Kwa maneno yake mwenyewe Kakobe anasimulia, “Sauti hii iliupondaponda moyo wangu, na kutetemesha mifupa yangu yote.Nilikuwa sijiwezi. Wakati makutano walipoimba nyimbo za furaha za kusifu kuhitimisha mkutano, sikuweza kuimba nao, badala yake, nililia kwa uchungu kwa sauti yangu ya juu. Nilitubu utukukutu wangu wakutokutii wito wa Bwana, nakumshukuru kwa kunivumilia na nikayapokea mapenzi yake, na nikasema, Ni hapa Bwana, nitumie Upendavyo. Kisha Roho wa Bwana akinijaa kwa uweza mkuu, na ghafla nijazwa nguvu ya Roho Mtakatifu; ujasiri, imani na utashi wa ndani kwa ndani wa kuhubiri Neno na kuwaombea wagonjwa na wenye uhitaji. Sikuweza kusubiri siku nyingine kulihubiri Neno Lake katika Mikutano ya Miujiza ya Uponya!”
Baada ya maandalizi muhimu ya kiroho, siku iliwadia.Hiyo ilikuwa Agosti 3, 1988; wakati Kakobe alipoanza safari yake ya uhubiri. Na timu yake ya wainjilisti,Gospel Evangelistic Team (GET), alienda mikoani kuanzisha mikutano mfululizo ya miujiza ya uponyaji, kwa mialiko kutoka makanisa mbalimbali ya Kipentekoste. Alifanya jumla ya mikutano ya wazi kumi Tanga, Kilimanjoro, Tabora, Mbeya, Pwani na Dar-Es-Salaam; nchini Tanzania.Akizungumzia mafanikio ya mikutano hii, mchungaji mmoja mkongwe alisema, “Hii mikutano kumi ya kwanza katika huduma yake imethibitisha kuitwa kwake.” Katika mikutano yote hii, mwitikio ulikuwa juu ya wastani maradufu.Mamia ya watu walimpokea Yesu Kristo, katika kila mkutano, na miujiza mingi ilitokea.
Akizungumzia miujiza ya ajabu, iliyotokea katika mikutano yake kumi ya kwanza ambayo hawezi kuisahau; Askofu Zakaria Kakobe alisema hivi, “Siwezi kuisahau miujiza miwili ya ajabu.Wa kwanza ni muujiza wa ajabu ambao Bwana alifanya katika mkutano niliofanya katika viwanja vya soko la kijiji cha Hedaru, mkoani Kilimanjaro; kuanzia Jumamosi, Agosti 13 hadi Jumatatu, Agosti 15, 1988. Mkutano huu ulikuwa umefadhiliwa Swedish Free Mission Church.Katika siku ya kwanza ya mkutano, wanakijiji walikuwa wagumu kuja karibu na viwanja vya mkutano kwa sababu hawakuamini katika miujiza; ndipo ghafla, nikawa nimejazwa aina flani ya imani isiyo ya kawaida iliyonitaka kuzungumza na watu waliokuwa kwa mbaali, na kuwaambia kumleta kiwete yeyote aliyefahamika kwa wanakijiji wote, na mara tu baada ya maombi kiwete huyo atainuka na kutembea.
Maeneo ya jirani tu , palikuwa na mwanamke ambaye alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 40, alikuwa ni kiwete toka tumboni mwa mama yake. Wanakijiji wote walimfahamu mama huyu. Walimpeleka kokote alikotaka kwenda kwa sababu hakuweza kujikokota wala kutambaa, achilia mbali kusimama mwenyewe na kutembea! Kwa harakaharaka walimleta karibu yangu, na wakasema, “Mhubiri, kama mama huyu atasimama na kutembea, basi tutaamini mahubiri yako” Kisha nikasema, “Kitu flani kisicho cha kawaida kinaenda kutokea, hapahapa, sasa hivi! Nawasubiria tuu watu wote waliosamama huko mbali.Tafadhali jongeeni karibu, na muone muujiza huu kwa macho yenu wenyewe.”Punde tuu, baada ya viwanja vya mkutano kufurika mamia ya watu ambao waliokuwa mamejaa shauku. Ndipo nikasema kwa ujasiri, “Mama huyu anakwenda kuamka na kutembea sasa hivi.” Baada ya kusema maneno haya uoga uliniingia, nilitetemeka, na mifupa yangu yote ilikuwa ikitetemeka. Aina hii ya utumishi ilikuwa ni mpya kabisa kwangu! Nilikuwa najifunza somo la namna ya kutumia karama za Roho Mtakatifu; katika Shule ya Roho Mtakatifu.Kisha nikasikia sauti ndani yangu ikisema, “Leo, utaaibishwa kwa sababu umesema kitu ambacho hakiwezekani. Utumishi wako unakwenda kuchafuliwa mara moja.”
Punde baadae, nilimuona mmoja wa nilioambatana nao, aliyekuwa akicheza kodiani, kabla sijachukua amdhabahu kuhubiri; taratibu akiondoka kuificha nafsi yake, Kisha nikasikia sauti tulivu ndani yangu ikisema, Usiogope, mtumishi wangu, maana Niko pamoja nawe. Sema neno la maombi tu na Nitafanya yanayobaki” Sauti mpya ilinifanya niisahau ya mwanzo, lakini nikaamua kufumba macho wakati nikiomba, ili nisione yaliyokuwa yakiendelea eneo hilo. Ndipo nikasema neno la maombi. Nilipomaliza kuomba, niliamua kuacha macho yangu yamefumba, ili nisione yaliyoendelea. Kisha ukafuata ukimya mfu, na kisha baadae, vifijo, na kelele kuu- aina ya pekee ya juu ya kuimba kwa tetemo inayotumiwa sana na wanawake Afrika na katika tamaduni nyingine, kama ishara ya furaha-iliyonifanya nifungue macho! Na unajua nini!Yule mama alisimama kwa miguu yake kwa mara ya kwanza katika maisha yake na kuanza kutembea. Umati ulikuwa umepamba moto kwa kelele za shangwe na kelele za haleluya! Taarifa za muujiza zilisamba kwa kasi kwa kuongea kwa watu kulikofanya watu wajae toka pande zote hata yule mcheza kodiani alitoka mafichoni! Kila mmoja alitaka kuona muujiza kwa macho yake wenyewe! Yesu alikuwa hai na halisi kwa kila mwanakijiji, na baada ya hapo wanakijiji waliamini kila neno lililohubiriwa. Miujiza ya kustajabisha iliendelea kuwa mada ya kijiji kwa miaka kadhaa baada ya mkutano.Pia, muujiza uliamsha imani yangu na kunifanya kumhubiri Yesu katika mikutano iliyofuata imani kubwa moyoni mwangu, isiyowahi kutokea kabla.
No comments:
Post a Comment