11 important things about Abraham Lincoln - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Monday, February 12, 2018

11 important things about Abraham Lincoln

February 12, 1809, alizaliwa aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln . Abraham Lincoln alikuwa maarufu sana wakati wa utawala wake hasa kwa kuthamini haki za wanawake na kupiga vita baishara ya utumwa nchini Marekani na duniani kwa ujumla.



Haya ni baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusu kiongozi huyo mkubwa wa Marekani, ambaye ameacha alama kubwa kwa nchi hiyo na dunia kwa ujumla.
1.Abraham Lincoln wakati wa utawala wake alipinga biashara ya watumwa nchini Marekani.
2.Wakati wa utawala wake, Abraham Lincoln alikuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kuthamini haki za wanawake, na kuamini kuwa wanawake pia wana haki ya kupiga kura, ingawa mpaka anauawa aliacha bado wanawake hawaruhusiwi kupiga kura.
3. Abraham Lincoln alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani kutokea katika chama cha Republican, chama ambacho anatokea Rais wa sasa Donald Trump.
4. Abraham Lincoln hakuwa na elimu maalum, alikuwa akijisomesha mwenyewe nyumbani lakini alikuwa na uwezo mkubwa kwenye kujifunza (Kwa ufupi hakuwa na taaluma yoyote)
5. Lincoln aliuawa na muigizaji John Wilkes Booth ambaye pia alikuwa shabiki yake mkubwa, siku ya Ijumaa Kuu mwaka 1865 , alipoenda kuangalia onyesho lao kwenye theatre.
6. Mtoto wa Abraham Lincoln, Robert Lincoln aliokolewa kwenye ajali ya treni na Edwin Booth, ambaye ni kaka wa muuaji wa baba yake.
7. Mama yake Abraham Lincoln alifariki baada ya kunywa sumu aliyowekewa kwenye maziwa, wakati Abraham Lincoln akiwa na miaka 9.
8. Abraham Lincoln alikuwa na tatizo la msongo wa mawzo, hivyo alikuwa habebi vitu vya ncha kali, akihofia kujidhuru.
9. Abraham Lincoln hakuamini kuwa watu weusi wana haki sawa na watu weupe (Alikuwa mbaguzi)
10. Lincoln alikuwa Rais wa kwanza wa Marekani ambaye sura yake iliwekwa kwenye sarafu (Ilikuwa kwenye sarafu ya senti 1)
11. Abraham Lincoln aliweka nyaraka zake muhimu chini ya kofia yakealiyokuwa akiipenda zaidi.
12. Kizazi cha Abraham Lincoln kimepotea kabisa, kwani watoto wake wake wote walishafariki, mtu wa mwisho wa kizazi chake alifariki mwaka  1985

No comments:

Post a Comment