Kuizunguka Afrika nzima kwa pikipiki - mambo matatu niliyojifunza - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Friday, January 26, 2018

Kuizunguka Afrika nzima kwa pikipiki - mambo matatu niliyojifunza

Mwendesha Pikipiki kutoka Uarabuni ameamua kuizunguka Afrika nzima anakusudia kufanya ziara yake katika nchi 47, akianzia safari yake nchini Oman.
Maher Al Baruan amepania kuweka historia ya kuwa raia wa kwanza wa Oman kuizunguka Afrika akitokea kwenda kusini kupitia mashariki kisha atapanda Oman kupitia Magharibi mwa Afrika.
Safari yake ilianzia nchini Oman mnamo mwezi wa saba mwaka 2017.
Mpaka sasa amekwisha safiri kwa miezi 7 na anasema safari yake itachukua zaidi ya mwaka kuikamilisha.
Wahenga wanasema, msafiri kafiri na mwenda pole hajikwai.
Lakini je, amejifunza nini katika safari yake? Akiwa mjini Bujumbura Maher Al Baruan ameelezea mambo matatu ambayo amejifunza kuhusu Afrika.

1. Usalama

Usalama ni jambo muhimu katika safari yoyote.
Changomoto kubwa Maher Al Baruan anasema anajihisi yuko katika hali ya hatari anaposafiri kwa sababu hajui atakutana na nani.
Anasema hata wanyama pori huwa ni jambo la kujitahadharisha.
Hata hivyo, anaelezea kuwa hajawahi kupata kisa chochote cha kumdhuru.

2. Umakini wa sheria za barabarani
Maher Al Baruan amegundua kwamba waendesha pikipiki wengi ambao amewaona hawatilii maanani sheria za barabarani na hasa za usalama kwa kuvaa kofia ngumu.
'Ningewashauri waendesha pikipiki wafuate sheria za barabarani, wasivue kofia ngumu kwa sababu hizi zote ni kwa ajili ya usalama wao' ameelezea Maher Al Baruan.

No comments:

Post a Comment