Nabii Tito ajijeruhi kwa kujikata na wembe Tumboni - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Friday, January 26, 2018

Nabii Tito ajijeruhi kwa kujikata na wembe Tumboni

Tito Onesmo Machibya anayejulikana kama ‘Nabii’ Tito akiwa ameshikiliwa polisi kwa mahojiano amezua taharuki baada ya kujijeruhi kwa kujikata na wembe tumboni ambapo kumepelekea ashonwe nyuzi 25 katika zahanati ya polisi Dodoma.
Daktari wa hospitali hiyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Tito alifikishwa hospitali saa 9 mchana akiwa anavuja damu eneo la tumbo ”Ni kweli Tito alifikishwa hapa majira ya saa 9 mchana, tulimfanyia matibabu kwa kumshona nyuzi 25 kutokana na ukubwa wa majeraha hayo” amesema Daktari.
Mnamo Januari 22, 2018 kamanda wa polisi Dodoma, Gilles Muroto alisema wamemkamata nabii Tito kwa kosa la kueneza chuki ya kidini dhidi ya watu wengine kwa kurekodi vipande vifupi vya video na picha vyenye maudhui ya kukashifu dini nyingine, na kuleta chuki dhidi ya watu wengine na kurusha katika mitandao ya kijamii pamoja na kusambaza vipeperushi kinyume na kifungu cha sheria namba 129 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 na marekebisho yake ya 2002.
Hivyo baada ya matibabu hayo nabii Tito alirudishwa polisi kwa mahojianao zaidi.

No comments:

Post a Comment