uchambuzi wa kina wa sayansi unaonyesha kuwa Muingereza kutoka miaka 10,000 ya nyuma alikuwa na ngozi nyeusi na macho ya rangi ya samawati.
Watafiti kutoka jumba la ukumbusho wa historia asilia mjini London wamepata chembechembe za vina saba vya Cheddar Man, mifupa ya zamani zaidi ya Muigereza iliyogunduliwa mnamo 1903.
Watafiti kutoka chuo cha University College London r baadaye walitumia uchambuzi wa vina saba kusaidia kuunda upya uso wake.
Indhihirisha kwamba ngozi nyeupe mingonimwa Wazungu wa sasa ni jambo la miaka ya hivi karibuni.
Hakuna Muingireza wa kabla ya historia hii aliyewahi kuchambuliwa kwa namna hii.
Kutokana na hili, uchambuzi huu unatoa muanga muhimu kuhusu watuw a kwanza walioishi Uingereza.
Uchambuzi huo wa Cheddar Man - utachapishwa katika jarida na pia utaangaziwa katika makala ndefu ya televisheni kwa jina 'The First Brit, Secrets Of The 10,000-year-old Man'.
Mifupa ya Cheddar Man ilifukuliwa miaka 115 iliyopita katika pango la Gough, lililoko huko Cheddar Gorge . Utafiti uliofuata ulidhihirisha kwamba alikuwa na kimo kifupi akilinganishwana viwango vya leo - kiasi cha ft5 in5 - na huedna alifariki akiwa na takriban miaka 20.
Profesa Chris Stringer, mtafiti kiongozi wa jumba hilo la ukumbusho kuhusu asili ya binaadamu amesema: "NImekuwa nikifanay uchunguzi wa mifupa ya Cheddar Man kwa miaka 40
"Kwahivyo kuona sasa sura inayowezekana kuwa ya jamaa huyu - na nywele, uso na rangi ya macho na mwili, jambo ambalo hatungelifikiria miaka michache iliyopita, na licha ya hayo hilo ndilo linalooneshwana data za sayansi."
nyufa katika fuvu la kichwa zinaashiria huenda alifariki katika mazingira ya ghasia, haijulikani ni vipi alivyoishia ndano ya pango hilo, lakini inawezekana aliwekwa hapo na wenzake katika jamii anayotoka.
Watafiti katika jumba hilo la ukumbusho ya historia asilia walitoa DNA kutoka sehemu ya karibu na sikio. Awali wanasayansi Prof Ian Barnes na Dkt Selina Brace hawakuwa na uhakika kwamba wangepata DNA katika masalio hayo ya mifupa.
Lakini walibahatika. walijumuika na wanasayansi kutoka chuo cha (UCL) kufanyia uchunguzi matokeo waliopata ikiwemo jini inayohusiana na nywele, rangi ya macho na ngozi pia.
Cheddar aliyekomaa
Waligundua kuwa muingreza huyo alikuwa na nywele nyeusi - na uwezekano mdogo kwamba zilikuwa za ondo -macho ya rangi ya samawati na ngozi iliyo nyeusi .
Mchanganyiko huu huenda ni tukautambua kwa wepesi leo, lakini ndilo lililokuwa umbo la kawaida Uropa magharibi wakati huo.
Sio jambo la kustaajabisha kwamba utafiti huu umewavutia wengi katika mitandao ya kijamii.
Utafiti huu umefichua kuwa Cheddar Man alikuwa na uhusiano na waliokuwa anajulikana kama wawindaji na wakusanyaji wa Maghribi - waliofanyiwa uchunguzi Uhispania Luxembourg na Hungary.
Wasanii wa uholanzi Alfons na Adrie Kennis, walitumia matokeo ya jini na kuyaunganisha na vipimo vya mwili kutokana na picha za fuvu la kichwa. Matokeo yake yalikuwa ni muundo wa sura ya kizazi cha nyuma.
Huenda ngozi nyeupe ilianza kuonekana Uingereza kwa uhamiji kutoka mashariki ya kati miaka 6000 iliyopita. Idadi ya watu hawa waikuwa na ngozi nyeupe na macho ya rangi ya kahawia na kuingiliana na jamii kama anayotoka Cheddar Man.
"Huenda kuna vigezo vingine vinavyosababisha kupungua kwa rangi ya ngozi katika muda wa miaka 10,000 iliypita. Lakini huo ndio ufafanuzi wanaotumia baadhi ya wanasayansi," amesema Prof Thomas.
Matokeo ya utafiti huo pia yameonyesha kuwa Cheddar Man hakuweza kunywa maziwa akiwa mtu mzima. Uwezo huu ulisambaa baadaye katika kizazi kilichofuata.
Asilimia 10 ya kizazi cha wazungu wa sasa kinatokana na jamii kama ya Cheddar Man.
No comments:
Post a Comment