DIMBWI LA MAHABA: Namna ya kumtambua mwenza anayekufaa - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Friday, February 2, 2018

DIMBWI LA MAHABA: Namna ya kumtambua mwenza anayekufaa

NI jambo la kawaida wengi wetu kuingia kwenye uhusiano, huku tukiwa na matumaini kwamba wenza tulio nao watakidhi vigezo vyetu na hivyo kutufaa katika maisha yetu ya uhusiano.
Hata hivyo, ndani ya uhusiano huo hukabiliwa na mtihani mkubwa wa namna ya kumtambua mwenza uliye naye kama ndiye anayekufaa kuwa naye katika maisha yako yote.
Jambo la msingi, ni kuhakikisha unapokuwa kwenye uhusiano unaweka malengo yako kwa kuhakikisha mwenza uliye naye unamfahamu vyema na si tu kuangalia yale mambo yanayokupendeza wewe tu.
Kumbuka kuwa wengi wetu tunapokuwa kwenye uhusiano siku za mwanzoni hupenda kuficha tabia zetu na uhalisia wetu na kujaribu kila njia kuhakikisha unafanya matendo yanayompendeza mwenza wako tu.
Hivyo ni vyema kutoingia kichwakichwa kutokana na ukweli kuwa mvulana mtanashati au msichana mrembo unayemuona leo anaweza kuwa si mwaminifu au asiye na maadili na huenda katika uhusiano wenu huo huko mbeleni lazima atakuletea shida.
Hapa ndiyo maana nasema ni vyema ukawa mwangalifu kwani huenda ukaona tu mambo unayotaka kuona. Hakikisha unamtambua vyema mwenza wako kiuhalisia ndipo utajua anakufaa au la.
Jaribu kupima uhusiano huo kulingana na matukio, kwa maana ya inapotokea shida, furaha, ukiwa na fedha au ukiishiwa. Hayo ni machache tu yatakuwezesha kuona ni mwenza wa aina gani uliye naye kwenye uhusiano ulionao.
Hebu angalia inapotokea kukwaruzana mwenza wako ni mtu wa aina gani, anapenda kukusikiliza au anataka asikilizwe yeye tu hoja zake? Je analipuka kwa hasira na kuanza kutukana au anatoa fursa ya kusikilizana na kushauriana?
Yapo mambo mengi yanayoweza kukuonesha aina ya mwenza uliye naye na kukurahisishia kujua kama anakufaa au la. Kumbuka kuwa si rahisi kumpata mtu asiye na matatizo jambo la muhimu ni kujifunza kuvumiliana na kuheshimiana.

No comments:

Post a Comment