new news from the prison when he was arrested for a famous actress(LULU) - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Monday, February 12, 2018

new news from the prison when he was arrested for a famous actress(LULU)





IKIWA ni takriban siku 85 tangu staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aswekwe lupango katika Gereza la Segerea, Dar kwa kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mapya akiwa gerezani yameanikwa. Mapya hayo yamebainika baada ya gazeti hili kutaka kujua kinachoendelea kwa sasa kwenye maisha ya Lulu ambapo Jumapili iliyopita.
saa 6 mchana mwandishi wetu alitinga katika gereza hilo kwa lengo la kumuona na kuzungumza naye lakini alikumbana na vizingiti.
Akizungumza na mwandishi wetu, mmoja wa maafisa wa magereza aliyekutwa eneo la getini na kugoma kutaja jina lake akidai si msemaji alisema:
“Kwani wewe ni miongoni mwa wale wana familia wanaokuja kumuona? Hapa wanaoruhusiwa ni wale tu ambao ni wanafamilia vinginevyo labda uje nao.”
Hata hivyo, mwanahabari wetu alijaribu kumlainisha afisa huyo na kumuweka wazi nia yake ya kufika gerezani hapo ambapo ulifika wakati akafunguka mambo mbalimbali mapya kuhusu Lulu.
Alisema mrembo huyo kwa sasa ni shavu dodo, anaendelea vizuri na kifungo chake na tangu aingie gerezani, hajawahi kuugua.
“Yani kwa kweli amenenepa kabisa tofauti na hata alivyokuja. Anaendelea vizuri na hajawahi kuugua ugonjwa wowote tangu afike,” alisema ofisa huyo.
Alipopigiwa simu mama Lulu, Lucresia Kalugira ili kueleza juu ya hali halisi ya mwanaye huyo, alitokwa povu huku akidai kwamba hataki kusikia magazeti.
“Sitaki kusikia habari za magazeti au waandishi wa habari maana mimi siyo supastaa na kuhusu mwanangu naombeni mmuache maana tayari yupo gerezani,” alisema mama Lulu.

No comments:

Post a Comment