Tiangong-1: Chombo cha China kuanguka duniani kikiwaka moto - HabariMagic

Breaking

Kerajaan

BANNER 728X90

Thursday, March 29, 2018

Tiangong-1: Chombo cha China kuanguka duniani kikiwaka moto

Haki miliki ya
Chombo cha anga za juu cha China kwa jina Tiangong-1 ambacho kimekuwa kikitumiwa kama maabara kinatarajiwa kuanguka duniani mwishoni mwa wiki.
Kina urefu wa mita 10 na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.
China inasema imepoteza mawasiliano yote na chombo hicho jambo ambalo linamaanisha kwamba mwendo wake wakati kinadondoka kutoka anga za juu hauwezi kudhibitiwa.
Hata hivyo, wataalamu wanasema uwezekano wa vipande vya Tiangong ambavyo havitakuwa vimeteketea kabisa wakati vikifika ardhini kuanguka kwenye maeneo yenye watu wengi ni mdogo sana.
"Ukizingatia kwamba Tiangong-1 ina uzani wa juu sana, vipande vyao vimekazwa sana, kuliko ilivyo kwa vitu vingine ambavyo hurejea duniani kutoka anga za juu, kumekuwa na juhudi nyingi za kutumia mfumo wa rada kufuatilia mwendo wake na kukadiria ni wapi kitaanguka," anasema Richard Crowther, mhandisi mkuu katika Shirika la Anga za Juu la Uingereza.
"Sehemu kubwa ya chombo hiki inatarajiwa kuungua kikiingia ndani ya anga ya dunia kutokana na kushika kiwango cha juu cha joto. Uwezekano mkubwa ni kwamba vipande ambavyo vitasalia baada ya hapo vitaanguka mahali baharini.

No comments:

Post a Comment